1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiMashariki ya Kati

Israel yaiataka ICJ kutupilia mbali kesi dhidi yake

Grace Kabogo
12 Januari 2024

Israel imewataka majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ, kutupilia mbali kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini, ambayo inaitaka mahakama hiyo kuiamuru Israel kusitisha operesheni za kijeshi katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4bBHe
Uholanzi | Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ
Mshauri wa masuala ya Kisheria wa Israel Tal Becker akiwa katika mahakama ya ICJPicha: Thilo Schmuelgen/REUTERS

Ikijibu hoja zilizowasilishwa jana na Afrika Kusini mbele ya mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa, Israel imesema madai ya kusitisha mashambulizi dhidi ya kundi la Hamas huko Gaza hayana msingi wowote.

Mshauri wa masuala ya sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel, Tal Becker amesema mahakama ya ICJ, haina mamlaka chini ya Mkataba wa Mauaji ya Kimbari kuiamuru kusitisha kampeni yake ya kijeshi Gaza.

Soma pia:Israel yaanza kujitetea kuhusu madai ya mauaji ya kimbari ICJ

Aidha, Wakili wa Israel, Malcolm Shaw amesema operesheni yake dhidi ya Hamas sio mauaji ya kimbari. Shaw amesema Afrika Kusini imesimulia tu nusu na yale yanayotokea Gaza. Israel imekanusha vikali madai hayo dhidi yake.