Israel Gaza
17 Juni 2010Jerusalem.
Mkutano wa baraza la mawaziri la Israel kuangalia ulegezaji wa nchi hiyo kuizingira Gaza, jana umemalizika bila kupata uamuzi. Hii imetokea licha ya ripoti za hapo kabla kuwa mawaziri hao walikuwa wapige kura kwa pendekezo lililotolewa na waziri mkuu Benjamin Netanyahu na mjumbe kwa ajili ya mashariki ya kati Tony Blair. Afisa wa serikali amethibitisha kuwa mazungumzo hayo yamemalizika baada ya karibu saa nane, ambapo mawaziri hao 15 watakutana tena leo Alhamis kwa ajili ya majadiliano zaidi juu ya suala hilo. Israel imepata mbinyo mkali kutoka jumuiya ya kimataifa kufuatia uvamizi meli za misaada iliyokuwa inakwenda Gaza uliosababisha watu kadha kuuwawa mwezi uliopita.