1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Norway, Ireland na Uhispania zatambua Palestina kama dola

22 Mei 2024

Norway, Ireland na Uhispania zimeitambua Palestina kama dola katika hatua ya kihistoria iliyochukuliwa na nchi hizo tatu hii leo Jumatano.

https://p.dw.com/p/4g8Q6
Norway itaitambua Palestina kama taifa
Waziri Mkuu wa Norway, Jonas Gahr Store akitoa mtazamo wa taifa lake kuhusu PalestinaPicha: Erik Flaaris Johansen/NTB/dpa/picture alliance

Waziri Mkuu wa Norway Jonas Gahr Stoere amesema hakuwezi kuwa na amani Mashariki ya Kati bila kuwepo suluhu ya madola mawili

Ireland nayo kupitia Waziri wake Mkuu Simon Harris imesema imechukua hatua hiyo iliyoitaja ya kihistoria kwa nchi yake na watu wa Paletina, kama njia ya kusaidia kupata suluhu katika mzozo wa Israel na Hamas ulioanza Oktoba 7. Utambuzi rasmi utafanyika tarehe 28 Mei.

Wakati huo huo waziri wa mambo ya nchi za nje wa Israel Israel Katz amewaamurumabalozi wa Ireland na Norway kurejea nyumbani mara moja kufuatia mataifa hayo kuitambua Palestina kama dola huru. Kiongozi wa Palestina Mahmood Abbas amekaribisha uamuzi huo na kuyataka mataifa mengine kuchukua hatua kama hiyo.