Heiligendamm: Russia yasubiri jawabu kuhusu kituo cha kukinga makombora. | Habari za Ulimwengu | DW | 09.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Heiligendamm: Russia yasubiri jawabu kuhusu kituo cha kukinga makombora.

Russia imesema inatarajia jawabu la kuridhisha kutokana na pendekezo ililolitoa la kushirikiana kujenga kituo cha kukinga makombora barani Ulaya.

Afisa mmoja mkuu wa Russia amesema Rais George W. Bush amevutiwa na mapendekezo ya Russia kwamba Marekani ijenge kituo hicho nchini Azerbaijan.

Rais wa Russia, Vladmir Putin, alitoa mapendekezo hayo siku ya Alhamisi iliyopita baada ya kupinga vikali mpango wa Marekani wa kujenga kituo hicho nchini Poland na Jamhuri ya Czek.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com