GAZA.Israel yazidisha mauaji Palestina | Habari za Ulimwengu | DW | 03.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA.Israel yazidisha mauaji Palestina

Wanachama wanne wa chama kinachotawala nchini Palestina cha Hamas wameuwawa mapema leo katika shambulio la kombora dhidi ya gari walilokuwa wakisafiria katika mji wa Gaza.

Katika operesheni nyingine wapiganaji wa Kipalestina watano wameuwawa wakati wa mapigano alfajiri leo katika mji wa Beit Hanoun.

Wanajeshi wa Israel wameuzingira msikiti mmoja katikati ya mji wa Gaza ambapo inaaminiwa kundi la wapiganajaji wa Palestina wamo ndani ya msikiti huo.

Waziri mkuu wa Palestina Isamil Haniya ameitaja operesheni hiyo ya majeshi ya Israel kuwa ni mauaji ya halaiki.

Takriban wapalestina 20 wameuwawa katika mji wa Beit Hanoun na vitongoji vyake tangu siku ya jumatano katika operesheni ya majeshi ya Isral kujibu mashambulio ya roketi yanayofanywa na wapiganaji wa Kipalestina.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com