Bush na Merkel wanazungumza | Matukio ya Kisiasa | DW | 11.06.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Bush na Merkel wanazungumza

Rais George Bush wa Marekani, aliyewasili hapa Ujerumani jana

default

Rais Bush na Kansela Merkel mjini Berlin


Ziara ya George Bush hapa Ujerumani, ambayo itakuwa ya kuaga kabla ya kuacha urais miezi sita hivi kutoka sasa, itadumu masaa 20. Hii ni ziara ya kudhihirisha pia kwamba yeye sio tu mshirika muhimu wa wa Ulaya, lakini pia wa Kansela Merkel. Uhusiano baina ya watu hao wawili ni ulio bora, ukilinganisha na ule na wa Kansela wa zamani Gerhard Schroader ambaye alipinga kabisa kujiingiza Marekani kijeshi nchini Iraq. Picha za Bush na Merkel zinaenda pamoja, anasema balozi wa Marekani mjini Berlin, William Timken:


"Chini ya uongozi wa Merkel na Bush, uhusiano baina ya Ujerumani na Marekani ni mzuri sana, nchi mbili hizo zinafanya kazi vizuri kwa pamoja."


Mwaka jana George Bush alimwalika Bibi Merkel atembelee shamba lake huko Texas, hivyo kutoa heshima maalum kwake. Kabla ya hapo, mwezi Januari mwaka jana wote wawili walikutana katika mkoa wa Mecklenburg-Vorpommern, anakotokea Bibi Merkel na huko wakala pamoja nyama ya kuchoma. Uhusiano huo mzuri wa watu hao wawili umemwezesha Bibi Merkel kutoa lawama zake kuhusu siasa za Bush kuelekea masuala ya mazingira na hali ya hewa duniani. Kama George Bush anatilia maanani lawama hizo ni suala jingine, anasema Karsten Voigt, mratibu wa serekali y a Ujerumani kuhusu uhusiano baina ya Ujerumani na Marekani:


+Sisi kwa Marekani si muhimu hivyo, ukilinganisha na Marekani ilivyo muhimu kwetu. Katika uhusiano huo, Marekani maisha inauliza: Jee Ujerumani ni muhimu kwetu katika kutanzuwa matatizo? Na Wajerumani maisha wanauliza: Vipi tunaweza kuwa na ushawishi na kusikilizwa na mshirika mwenye uzito mkubwa kuhusu fikra zetu?"


Wanasiasa wa Kijerumani hawajasikilizwa na George Bush juu ya vita vya Iraq na kuhusu gereza la Guantanamo, na ndio maana ziara ya sasa ya Bush imefuatilizwa na lawama kutoka wahakiki. Wanasiasa wa kutoka vyama mbali mbali hapa Ujerumani wanasema George Bush ameichafua sura ya Marekani duniani. Lawama hizo hii leo hatakumbana nazo uso kwa uso, kwani atabakia tu ndani ya jumba la wageni la serekali huko Meseberg, ambalo limewekewa ulinzi mkali.


Lakini jana baada ya mkutano wa kilele wa saa tatu baina ya Umoja wa Ulaya na Marekani huko Slovenia, George Bush alisema anaamini katika kipindi chake kilichobaki cha urais kutapatikana mkataba wa dunia kuhusu mabadiliko ya hewa duniani. Lakini kuhusu mabishano yake na utawala wa Iran, hajatafuna maneno:

"Iran na silaha za kinyukliya itakuwa hatari sana kwa amani ya dunia."


Alasiri ya leo George Bush ataelekea Roma, Italy.
 • Tarehe 11.06.2008
 • Mwandishi Othman, Miraji
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EHlg
 • Tarehe 11.06.2008
 • Mwandishi Othman, Miraji
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EHlg
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com