1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Israel kuamua kuhusu hukumu ya kifo kwa Wapalestina

30 Machi 2026

Bunge la Israel kuamua kuhusu hukumu ya kifo kwa Wapalestina wanaowaua Waisraeli Ukingo wa Magharibi.

https://p.dw.com/p/5BN2G
Bunge la Israel laanza kuujadili muswada wa kuongeza adhabu kwa Wapalestina watakaopatikana na hatia ya kuwaua Waisraeli huko Ukingo wa Magharibi hadi hukumu ya kifo.
Bunge la Israel laanza kuujadili muswada wa kuongeza adhabu kwa Wapalestina watakaopatikana na hatia ya kuwaua Waisraeli huko Ukingo wa Magharibi hadi hukumu ya kifo.Picha: dpa/picture alliance

Bunge la Israel linatarajiwa kujadili muswada utakaohalalisha hukumu ya kifo kwa Wapalestina watakaokutikana na hatia ya kuwaua Waisraeli katika Ukingo wa Magharibi.

Bunge hilo limeanza kuujadili muswada huo siku ya Jumatatu.

Kupitishwa kwa mswada huo kutakuwa kilele cha msukumo wa miaka mingi wa siasa za mrengo mkali wa kulia nchini Israeli wa kuongeza adhabu kwa Wapalestina waliohukumiwa kwa makosa ya siasa za kizalendo dhidi ya Waisraeli.

Aidha itakuwa ushindi kwa waziri wa usalama wa Israeli, Itamar Ben-Gvir, ambaye pia ni kiongozi wa chama cha kidini kilichowasilisha muswada huo.

Wapinzani wa muswada huo wanautaja kama wa kibaguzi wa rangi, katili na usioweza kuzuia mashambulizi kutoka kwa wanamgambo wa Kipalestina.