1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken: Uchaguzi ufanyike kama ulivyopangwa Senegal

14 Februari 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ahimiza uchaguzi Senegal ufanyike haraka iwezekanavyo huku akionesha wasiwasi kuhusu kucheleweshwa kwake baada ya kuwasiliana kwa njia ya simu na Rais Macky Sall.

https://p.dw.com/p/4cMuc
Maandamano ya Senegal katika mitaa ya Dakar
Waandamanaji wanapinga uamuzi wa Rais Macky Sall wa kuahirisha kura ya Februari 25.Picha: Stefan Kleinowitz/AP Photo/picture alliance

Kwa mujibu wa Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Matthew Miller, ameweka wazi kuwa wangependa kuona uchaguzi unafanyika kama ulivyopangwa.

Miller pia alisema kuwa Marekani inawasiwasi mkubwa kuhusu hali katika taifa hilo la Afrika Magharibi, ambapo mamlaka Jumanne(13.02.2024) ilizuia mtandao wa simu na kupiga marufuku maandamano.

Kama uchaguzi usipofanyika Februari 25, basi ufanyike haraka

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken
Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken akizungumza wakati wa mkutano wake na Rais wa Israel Isaac Herzog katika Makazi ya Rais mjini Jerusalem, Israel, Jumatano, Februari 7, 2024.Picha: Mark Schiefelbein/AP/picture alliance

Miller ameongeza kwa kusema Blinken anahimiza uchaguzi ufanyike kwa wakati na ikiwa hautafanyika Februari 25, ungepaswa kufanyika haraka iwezekanavyo baada ya hapo.

Rais Sall amesogeza mbele uchaguzi wa Februari 25, na kusababisha mzozo wa kisiasa nchini Senegal, ambalo kijadi ni thabiti na kutolewa mfano na Blinken kama demokrasia bora kwa Afrika katika ziara yake ya 2021.

Umoja wa Mataifa wataka haki ya kuandamana iheshimiwe

Machafuko ya Senegal huko Dakar
Mwandamanaji aliyevalia bendera ya Senegal kuzunguka ishara za mwili wake wakati wa mapigano na polisi huko Dakar mnamo Februari 9, 2024.Picha: GUY PETERSON/AFP

Katika hatua inayofanana na hiyo, Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema haki ya Wasenegal kuandamana kwa amani lazima iheshimiwe.

Kauli hiyo ni baada ya mamlaka ya taifa hilo la Afrika kupiga marufuku maandamano kufuatia kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais. Msemaji wa Guterres, Stephane Dujarric amesema wana wasiwasi sana kuhusu maendeleo ya kwa hali ya amani nchini Senegal.

Soma zaidi: Wabunge wakamatwa wakipinga kuahirishwa uchaguzi Senegal

Aidha amesema ni muhimu sana kwamba Wasenegal wote wawe na haki yao ya kuandamana, kuheshimiwa kwa amani, akitaka hali hiyo "isuluhishwe kupitia njia zilizowekwa za kikatiba ya taifa hilo.

 

Chanzo: RTR