1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAmerika ya Kaskazini

Biden kuwania tena urais 2024

Sudi Mnette
10 Aprili 2023

Rais Joe Biden wa Marekani amesema ana mpango wa kuwania urais wa Marekani katika uchaguzi ujao wa mwaka 2024 ingawa hakuwa tayari kutangaza hatua hiyo katika kipindi hiki.

https://p.dw.com/p/4PsbG
Joe Biden Porträt Kandidatur
Picha: Kevin Dietsch/Getty Images

Biden ameyasema hayo kupitia kituo cha  kituo cha televisheni cha Marekani cha NBC ikiwa ni kabla ya hafla maalumu ya Pasaka ya Ikulu ya Marekani.

Katika hatua nyingine, waziri wake wa mambo ya nje, Antony Blinken, juma hili anaanza ziara katika mataifa ya Uingereza, Ireland, Vietnam, na Japan. Akiwa Hanoi atafanya mazungumzo na maafisa wa Vietnam na kuhudhuria hafla ya kutimiza miaka 10 ya mahusiano thabiti kati ya Marekani na Vietnam.

Pia atahudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa kundi la mataifa saba tajiri duniani - G7 huko Japan, baada ya kumsindikiza Biden katika safari yake ya Aprili 11 hadi 14 ya Uingereza na Ireland.