1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden atofautiana na Trump, Kenosha.

Lilian Mtono
4 Septemba 2020

Mgombea wa urais kupitia chama cha Democratic Joe Biden amewaambia wakazi wa Kenosha katika jimbo la Wisconsin kwamba hali tete iliyojitokeza katika siku za karibuni kwenye eneo hilo.

https://p.dw.com/p/3hzQI
USA Kenosha Besuch Joe Biden
Picha: Reuters/K. Lamarque

Machafuko yameukumba mji wa Kenosha kufuatia tukio la polisi kumpiga risasi Mmarekani mweusi Jacob Blake, inaweza kuwasaidia wamarekani kukabiliana na ubaguzi wa kimfumo uliodumu miongo kadhaa nchini humo, matamshi yanatoafutiana kabisa na rais Donald Trump. 

Biden amesema kwenye kanisa la Kilutheri la Grace ambako alikutana na viongozi wa eneo hilo baada ya kikao cha faragha na Blake pamoja familia yake kwamba hatimaye Wamarekani sasa wamefikia mahali ambapo watatakiwa kushughulikia alichokiita ''dhambi ya asili'' ya taifa hilo, utumwa pamoja na mabaki yake yote.

Ziara hiyo iliashiria safari ya kwanza ya makamu huyo wa rais wa zamani kwenye eneo linalokabiliwa na machafuko katika jimbo la Wisconsin, kama mgombea mteule wa urais kupitia chama cha Democratic na ilikuwa kielelezo cha wazi kabisa kinachoonyesha tofauti kati yake na Trump.

Wakati Biden akiwa ametumia zaidi ya saa moja akiwa na familia ya Blake, Trump hakuthubutu hata kumtaja Blake alipokuwa ziarani mjini Kenosha siku ya Jumanne. Huku Biden akisema matatizo yanayoshuhudiwa katika mfumo wa sheria yalianza enzi ya utumwa nchini Marekani, Trump alikataa kukiri kuhusu ubaguzi wa kimfumo na badala yake akaonyesha kuunga mkono waziwazi vyombo vya sheria, huku akiyataja machafuko hayo kuwa ni ugaidi wa ndani.

USA Präsident Trump in Kenosha
Rais Donald Trump anayafananisha machafuko ya Kenosha na ugaidi wa ndani, na kutofautiana na Biden.Picha: Reuters/L. Mills

Biden amemkosoa Trump kutokana na madai yake dhidi ya waandamanaji, kujitetea kwamba anatumia sheria na kukanusha kwamba Wamarekani wenye ngozi za nyeusi wanakabiliwa na vizingiti, tofauti na weupe. Akasema, matamshi ya rais yanaweza kuharibu ama kuleta amani.

Alisema "Kama ninaweza kutoa hoja ya kawaida, matamshi ya rais yana uzito, haijalishi ni mazuri, mabaya au ya kujali, ni muhimu. Haijalishi rais ana uwezo gani au hana uwezo, anaweza kupeleka taifa vitani. Anaweza kuleta amani. Anaweza kufanya masoko kupanda au kushuka. Na anaweza kufanya vitu ambavyo nimeona vinaweza kuleta mabadiliko kwa kile anachosema tu."

Blake bado yuko hospitali baada ya kupigwa risasi mgongoni mara saba na polisi mzungu katika mji wa Kenosha, wakati walipokuwa wakijaribu kumkamata Agosti 23. Tukio hilo ni la karibuni la polisi kukabiliana na mtu mweusi na kuibua maandamano makubwa. Tukio la awali lilikuwa na mauaji ya George Floyd katika mji wa Minneapolis ambalo pia lilisababisha maandamano makubwa mnamo mwezi Mei.

Nje ya kanisa hilo, mjomba wa Blake alifananisha ziara za wagombea hao wawili akisema, Trump hakuuliza chochote kuhusu ndugu yake wakati akiwa ziarani Kenosha na kumuita Biden kuwa ni mtu anayeunganisha watu na kukisifu chama cha Democratic kwa kuleta mabadiliko katika mfumo wa sheria hata kabla ya kuombwa kufanya hivyo.

Soma ZaidiAhadi ya Biden kuhusu utulivu kujaribiwa mjini Kenosha

Mashirika: APE