1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bernard Membe arejea CCM

Josephat Charo
29 Mei 2022

Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania na mgombea urais wa chama cha ACT Wazalendo Bernard Membe amerudishiwa kadi ya uanachama wa chama cha mapinduzi CCM (29.05.2022)

https://p.dw.com/p/4C1Ak
Tansania Bernard Membe erhält seine CCM-Mitgliedskarte in Chiponda Rondo in Lindi, von Shaka Hamdu Shaka
Picha: Salma Mkalibala/DW

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa imemrejeshea kadi ya uanachama aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye serikali ya awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bernard Camilius  Membe. Membe amerejea CCM akitokea chama cha ACT-Wazalendo alikohamia na kugombea nafasi ya urais kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi uliopita.

Zoezi hilo limefanywa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa Shaka Hamdu Shaka leo katika kijiji cha Chiponda Rondo,wilaya ya Lindi mkoani Lindi.

Shaka amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya Bernard Membe kuomba msamaha wa kurudishiwa uanachama baada ya kufukuzwa Februari 28, 2020 kutokana na kutuhumiwa kwa makosa ya kimaadili.

Membe ameiambia hadhira iliyojitokeza kushuhudia tukio hilo kuwa amerudi CCM kwa kuwa hakuna tena sababu za kumzuia kutokuwa mwanachama bila kufafanua kwa kina.

Salma Mkalibala