Bayern Munich na Leverkusen-Manchester United na City. | Michezo | DW | 28.11.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bayern Munich na Leverkusen-Manchester United na City.

Gebreselassie uwanjani Australian marathon.

Majogoo wa Hoffenheim kileleni.

Majogoo wa Hoffenheim kileleni.

Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wanachuana uwanjani wakati huu na Bayer Leverkusen kuamua nani ataibuka mabingwa wa nusu msimu.Viongozi wa Bundesliga-

Hoffenheim wako nyumbani leo wakiikaribisha Bielefeld.Katika Premier League-Ligi ya Uingereza kinyanganyiro kileleni kikiendelea kati ya Chelsea na Liverpool, mabingwa Manchester United wana miadi na Manchester City.

Kamati ya maandalio ya Kombe la dunia 2010 nchini Afrika Kusini yasema imeridhishwa na matayarisho yanavyokwenda vyema tangu kwa kombe la dunia hata kwa kombe la mashirikisho linaloanza Juni mwakani.

Bingwa wa rekodi ya dunia wa mbio za marathon -Gebrselassie anakimbia mbio zake za kwanza kesho huko Australia tangu kuiweka rekodi ya dunia mjini Berlin chini ya masaa 2 na dakika 4.

Bundesliga:

Mabingwa wa Ujerumani-Bayern Munich yaonesha upepo unavumia upande wao wakati huu,kinyume na pale msimu ulipoanza.Leo wana miadi na Bayer Leverkusedn,timu iliobadilishana usukani wa uongozi wa Ligi msimu huu na Hoffeheim,klabu iliopo sasa kileleni na iliotoka daraja ya pili. Munich inarudi uwanjani leo baada ya kutamba mwishoni mwa wiki iliopita mbnele ya Energie Cottbus na kati ya wiki majogoo wake 3-akina Luca Toni,Miroslav Klose na Franck Ribbery, kutamba na kuizaba Buckarest nje ya Champions League-kombe la klabu bingwa barani Ulaya.

Leverkusen ina kibarua kigumu leo,kani tayari mwishoni mwa wiki iliopita ilikiona kilichomtoa kanga manyoya mbele ya timu inayoburura mkia ya Armenia Bielefeld kwa mabao 2:1.Isitoshe, Leverkusen ingawa imeaanza uziri msimu huu, mara ya mwisho kutamba mbele ya Bayern Munich,ilikua 2004. Tangu mabingwa Munich hata mahasimu wao leo Bayer Leverkusen ana pointi 28-pointi 3 nyuma ya viongozi wa Ligi-Hoffenheim. Hoffenheim wanatamba leo nyumbani mbele ya timu ile ile ilioingoa meno Leverkusen-Armenia Bielefeld. Wakishinda leo na Munich ikiitoa everkusen, Hoffenheim itabakia kileleni hadi mwishoni mwa wiki ijayo itakapokumbana na Bayern Munich kuamua ni ipi kati yao nik mabingwa wa nusu-msimu kabla likizo ya X-masi na mwaka mpya.

Lakini, Leverkusen inajivunia kikosi cha washambulizi wakali kama vile Patrick Helms aliejiunga mimu huu na Leverkusen kutoka FC cologne na Stefan Kiessling kutoka Nuremberg.Uchunguzi wa maoni ya mashabiki unaagua kuwa Hoffenheim itaibuka mabingwa wa nusu-msimu na sio Bayern munich. Berlin na FC Cologne.

Ama katika Premier League, Chelsea na Liverpool zingali zikitamba kileleni wakati Arsenal yaanza kukata tamaa ya ubingwa msimu huu.Taarifa zadai idadi ya mashabiki katika viwanja vya Premier League-ligi ya Uingereza imeshuka kwa kiasi cha mashabiki 920 kima cha wastani kwa kila mechi.Sababu pengine ni msukosuko wa fedha.

Wakati mahasimu 2 wa mtaani Manchester United na Manchester City wana miadi kesho,Chelsea wanakumbana na Arsenal.Hata changamoto hizi hazitazamiwi kusheheni sana kwa mashabiki. Liverpool imepatwa na mkosi wa kuumia stadi wao kutoka Spain, Torres.

MAANDALIO YA KOMBE LA DUNIA 2010:

Akizungumza na vyombo vya habari kati ya wiki hii, mwenyekiti wa kamatai ya Maandalio ya kombe lijalo la dunia nchini Afrika kusini,Danny Jordaan ,alisema wamefurahishwa na jinsi maandalio yanavyokwenda.

"Tangu kuanza kuuzwa kwa tiketi za kombe la mashirikisho-Confederations Cup mwishoni mwa wiki iliopita,tumeshauza tiketi 30.000 kupitia mtandao wa internet.Ni vigumu kusema jinsi uuzaji unavyokwenda sehemu nyengine,lakini tunatumai viwanja vitasheheni ."-alinukuliwa kusema Danny Jordaan.Jordaan akasema kwamba kamati yake imeidhinisha dala milioni 386.5 kugharimia mashindano hayo mawili.

"Tumepokea hivi punde kitita cha dala milioni 200 kutoka FIFA.Kwa kuwa kipimo cha kubadilisha sarafu kati ya Dola na Rand kimebadilika,hivyo tumetia mfukono fedha zaidi kuliko tungelipata iwapo fedha hizo zingetolewa mwaka jana."-aliongeza mwenyekiti huyo wa Kamati ya maandalio ya kombe la Dunia 2010.

Nae Katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke, amearifu kwamba, serikali ya Afrika Kusini itaruhusu mashirika mengi zaidi ya ndege kutua Afrika Kusini wakati wa Kombe la Dunia. Akasema pia kwamba, sasa hakuna lolote linaloweza kuhatarisha ama Kombe la Dunia au la mashirikisho. Katibu mkuu wa FIFA akaongeza kusema kwamba walichukua uamuzi barabara kuutoa Uwanja wa Port Elizabeth katika orodha ya viwanja vitakavyochezewa Confederations Cup Juni mwakani.

Kwani, Uwanja huo haungekuwa tayari kwa kombe hilo.Akihutubia waandishi habari waliojumuisha wale wa kimataifa ,Jordaan alisema anatumai waandishi hao watarejea makwao na imani. Kesho ni zamu ya Australian marathon na macho yakodolewa bingwa wa rekodi ya dunia mzee Haile Gebrselassie wa Ethiopia:

RIADHA:MBIO ZA AUSTRALIAN MARATHON:

Bingwa wa rekodi ya dunia wa mbio za marathon,Haile Gebrselassie, kwa mara ya kwanza tangu aivunje rekodi yake binafsi ya dumnia katika Berlin marathon Septemba mwaka huu, anarudi kesho uwanjani kukimbia katika Great Australian Run-mbio za masafa ya km 15.Gebrselassie,mwenye umri wa miaka 35 ni binadamu wa kwanza kukimbia marathon kwa muda usiopindukia masaa 2 na dakika 4.

Rekodi yake ya dunia mjini Berlin ni masaa 2 na dakika 3.59.Bingwa huyu wa Olimpik wa mita 10.000 mwaka 2000 huko Sydney,Australia na 1996 mjini Atlanta, alieweka rekodi yake ya 26 mjini Berlin, hakuondoa uwezekano wa kuzifikisha rekodi zake hadi 30 katika muda wake uliosalia wa kukimbia. selassie, aliungama jana kuwa hiyo ndio shabaha yake.

Muethiopiya huyu aliweka rekodi yake ya kwanza ya dunia mjini Hengelo,Holland, hapo 1994 alipokimbia masafa ya mita 5000 kwa muda wa dakika 12.56.96 atatoana kesho jasho na bingwa wa Jumuiya ya madola Samson Ramadhani wa tanzania,bingwa wa nusu-marathon kutoka Kenya Patrick M akau na Muaustralia Craig Mottram. Gebrselassie, bingwa mara 4 wa dunia wa mita 10.000 kutoka 1993 hadi 1999 amenadi kwamba yutayari kuanza changamoto na mkenya huyo Patrick Makau mwenye umri wa miaka 23 kwa 35 ya Gebrselassie.

Muaustralia Mottram, ameungama kwamba kasi itaua matumaini yake yoyote ya kumshinda bingwa wa dunia kutoka Ethiopia.Mottram hakuwahi pia kukimbia mbio zilizovuka masafa ya km 12 na hivyo kasi katika mbio za kesho itaamua mshindi.

Mbio hizo za km 15 kupitia barabara za mji wa Melbourne,zimevutia wanariadha 4000.Kwahivyo, si ajabu macho kesho yakakodolewa Melbourne.