1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Bunge la Marekani lapitisha muswada wa ukomo wa kukopa

1 Juni 2023

Baraza la wawakilishi limepitisha muswada unaungwa mkono na vyama viwili, juu ya kupandisha kiwango cha ukopaji wa serikali hadi dola trilioni 31.4.

https://p.dw.com/p/4S38X
USA | Capitol in Washington
Picha: Mandel Ngan/AFP/Getty Images

Kura hiyo ni hatua muhimu katika kuzuia hatari ya serikali ya nchi hiyo kushindwa kuyalipa madeni yake, hali ambayo inaweza kuiyumbisha nchi hiyo.

Rais Joe Biden amesema makubaliano hayo ni habari njema kwa watu wa Marekani na kwa uchumi wao. Sheria ya uwajibikaji wa kibajeti ilihitaji wingi mdogo wa kura katika baraza hilo la wawakilishi linalodhibitiwa na chama cha Republican.

Soma pia: Biden na Warepublican wakubaliana ukomo wa Deni la Taifa

Baada ya hapo muswada huo utapelekwa katika baraza la seneti, kabla ya kuwasilishwa kwenye meza ya rais ili usainiwe kuwa sheria.