1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden na Warepublican wakubaliana ukomo wa Deni la Taifa

28 Mei 2023

Rais Joe Biden wa Marekani na spika wa Baraza la Wawakilishi Kevin McCarthy wametangaza kufikia makubaliano ya kuongeza ukomo wa deni la taifa, uamuzi unao ondoa kiwingu cha Washington kushindwa kulipa deni lake.

https://p.dw.com/p/4Ruie
Ris Joe Biden na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, Kevin McCarthy
Ris Joe Biden na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, Kevin McCarthy Picha: Drew Angerer/Getty Images

Kwenye tarifa yake iliyotolewa saa chache zilizopita, rais Biden ameyataja makubaliano hayo kubwa "habari njema kwa umma wa Marekani, kwa sababu yatazuia taathira kubwa kwenye uchumi" iwapo taifa hiyo lingefikia hatua ya kushindwa kulipa madeni yake.

Spika McCarthy amesema "bado kuna kazi kubwa ya kufanywa" ikiwa ni pamoja na kuwashawishi wabunge kupitisha makubaliano hayo mnamo Jumatano inayokuja.

Hapo kabla wizara ya fedha ya Marekani ilitangaza Juni 5 kuwa tarehe ambayo serikali ya nchi hiyo ingeishiwa fedha za kulipia mahitaji yake na kuutumbukiza uchumi huo mkubwa duniani kwenye mparaganyiko.