BAMAKO:Rais Amadou ashinda kipindi cha pili madarakani | Habari za Ulimwengu | DW | 02.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAMAKO:Rais Amadou ashinda kipindi cha pili madarakani

Rais Amadou Toumani anadai ushindi wa kipindi cha pili cha urais baada ya kuzoa zaidi ya asilimia 70 ya kura katika uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa juma lililopita.

Matokeo hayo ni kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa na wawakilishi wake katika vituo vya kupigia kura.Upinzani nchini humo umeapa hapo jana kupinga katika mahakama ya katiba uchaguzi huo uliompa ushindi rais Amadou.

Waangalizi wa kimataifa wanasema uchaguzi ulifanyika kwa njia huru na haki.Hata hivyo matokeo rasmi bado hayajatangwazwa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com