BAGHDAD.Kituo cha televisheni cha Wassuni chavamiwa
12 Oktoba 2006Matangazo
Watu wenye silaha wamezivamia afisi za kituo cha matangazo ya televisheni kwa satellite mjini Baghdad na kuwauwa walinzi na wafanyakazi kiasi wanne.
Ripoti zinasema kwamba hujuma hiyo ilifanywa mapema leo asubuhi.
Kituo hicho cha televisheni cha Saabia ni cha Wassuni, hali inayoashiria huenda mauaji hayo yanahusiana na uhasama kati ya Wassuni na Washia.
Hakuna taarifa zaidi zilizopatikana.