1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Afrika Kusini yaitaka ICJ kuishinikiza Israel kuhusu Gaza

Amina Mjahid
7 Machi 2024

Afrika Kusini imewasilisha ombi la haraka kwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki ya ICJ, kuiamuru Israel kukubali misaada zaidi ya kibinaadamu katika Ukanda wa Gaza, huku ikitahadharisha juu ya kitisho cha baa la njaa

https://p.dw.com/p/4dFfx
Mahakama ya Kimataifa ya Haki - ICJ mjini The Hague
Afrika Kusini inasema Israel inakiuka sheria za kimataifa katika vita vyake dhidi ya Hamas huko GazaPicha: Selman Aksunger/AA/picture alliance

Afrika Kusini imewasilisha ombi la haraka kwaMahakama ya Kimataifa ya Haki ya ICJ, kuiamuru Israelkukubali misaada zaidi ya kibinaadamu katika Ukanda wa Gaza, huku ikitahadharisha juu ya kitisho cha baa la njaa.

Afrika Kusini imesema imerejea tena katika Mahakama hiyo iliyoko mjini The Hague, Uholanzi, kuwasilisha ombi hilo la haraka kufuatia Wapalestina kunyimwa haki ya kupata chakula na Israel.

Taifa hilo la Afrika limeishutumu Israel kuendelea kukiuka sheria za Umoja wa Mataifa za kuzuwia mauaji ya halaiki katika vita vinavyoendelea mjini Gaza.

Tangu kuanza kwa mapigano kati ya Israel na Hamas mnamo Oktoba 7, Wapalestina zaidi ya 30,000 wameuwawa, wengi wao wakiwa wanawake na watoto.