Abuja.Visima vya mafuta vyatekwa na watu wenye hasira. | Habari za Ulimwengu | DW | 26.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Abuja.Visima vya mafuta vyatekwa na watu wenye hasira.

Wanakijiji waliokuwa na hasira nchini Nigeria wamevamia na kuviteka visima vitatu vya mafuta vya kampuni ya Shell katika eneo la Delta.

Kampuni hiyo ya mafuta imesema kuwa, uzalishaji wa mafuta katika kila kisima unalazimika kusimamishwa.

Katika taarifa yake, kampuni ya Shell imesema kuwa, wanachama wa jumuiya ya Kula walivamia maeneo hayo ya visima hapo jana, wakilalamikia kampuni hiyo ya nishati kushindwa kufikia makubaliano ya kuwapa huduma.

Hadi hivi sasa hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na wafanyakazi wa visima hivyo baada ya tukio hilo.

Wakati huo huo wafanyakazi saba wa kigeni wa kampuni ya mafuta ya Exxon Mobil wameachiliwa huru salama baada ya siku 18 za kutekwa nyara.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com