Zelensky aishukuru Ujerumani kwa kuipa mifumo ya Ulinzi
3 Novemba 2025
Matangazo
Akiandika katika mtandao wake wa X, Zelenksy alimshukuru kansela wa Ujerumani Friedrich Merz, kwa msaada wa mifumo hiyo, akisema hii inaonesha namna nchi hiyo ilivyojitolea kuwalinda raia wa Ukraine.
Rais huyo wa Ukraine hakutoa taarifa zaidi juu ya msaada zaidi aliyopokea kutoka Ujerumani, lakini vyombo vya habari vinadai Ukraine ina mifumo 10 ya ulinzi wa anga ya Patriot iliyotengenezwa Marekani lakini kutumwa nchini humo kwa usaidizi wa Ujerumani.
Huku hayo yakiarifiwa waziri wa fedha wa Ujerumani Lars Klingbeil ametaka hatua kali zaidi zichukuliwe dhidi ya Urusi kuishinikiza kuachana na vita vyake Ukraine.