1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zanzibar yawavutia wawekezaji

Salma Said8 Desemba 2021

Kwa mara ya kwanza tangu kupatikana Uhuru wa iliyokuwa Tanganyika (Tanzania Bara) sehemu kubwa ya sherehe hizo zimefanyika Zanzibar kwa mikutano na makongamano kadhaa yanayolenga kuwavutia wawekezaji.

https://p.dw.com/p/43z9a
Wirtschaftsforum in Sansibar
Picha: Salma Said/DW

Mnamo Jumanne, Rais wa Zanzibar Daktari Hussein Ali Mwinyi alifungua kongamano kubwa la wawekezaji. 

Katika kongamano hilo la kuadhimisha miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika, ambalo linafikia kilele tarehe 9 kwa mkutano mkubwa utakaofanyika Dar es Salaam, Rais Daktari Hussein Mwinyi aliwaomba wawekezaji wakiwemo kutoka Misri na China waje kwa wingi kuwekeza kwa sababu kwa sasa mazingira ya uwekezaji ni mazuri yasiyokuwa na vikazo.

Rais Mwinyi amesema serikali zote mbili zinajitahidi katika kutengeneza mazingira mazuri ili kuwavutia wawekezaji na kuomba juhudi zaidi kuhakikisha mazingira rafiki yanabakia.

Ujumbe mkubwa wa kongamano hilo ni miaka 60 ya uhuru na maendeleo ya kiuchumi ambapo Rais Mwinyi alisema kuna maeneo mengi bado hayajafanyiwa kazi ikiwemo sekta ya mafuta.

Ujumbe mkubwa wa kongamano hilo ni miaka 60 ya uhuru na maendeleo ya kiuchumi
Ujumbe mkubwa wa kongamano hilo ni miaka 60 ya uhuru na maendeleo ya kiuchumiPicha: Salma Said/DW

Kwa upande wake waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu uwekezaji Geofreyy Mwambe watumishi wa serikali wanapaswa kuweka mazingira mazuri ili kuwavutia wawekezaji huku akiwavuta wawekezaji kwa kuisifia mazingira yaliyopo hivi sasa.

Hoja 11 zinazoelezea kero za Muungano wa Tanzania

Kongamano la Jumatano ni Mawaziri kutoka Tanzania bara na Zanzibar na wawekezaji wazalendo ambao mbali wamehudhuria ambapo Mkugenzi Mtendaji Jumuiya ya kitaifa ya wafanyabiashara Zanzibar, Hamad Hamad ametumia fursa hiyo kuhimiza mfungamano mwema kati ya wafanyabiashara wa Zanzibar na Tanzania ili kuimarisha sekta hiyo huku akisisitiza vikwazo vilivyobaki viondoshwe.

Maadhimisho ya miaka 60 pia yamehusu maonesho ya kibishara katika jiji la Zanzibar ambapo makampuni zaidi ya mia moja wanashiriki yakisimamia na taasisi ya biashara TAN TRADE' kwa mara ya kwanza Zanzibar ambapo msukumo wa sherehe hizi kufanyika Zanzibar ni kutokana na kuwa Rais wa sasa wa Muungano anatoka Zanzibar.