1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO: Ebola ilisababisha vifo vya watu 42 DR Kongo

2 Oktoba 2025

Shirika la afya Ulimwenguni limesema mripuko wa Ebola uliotangazwa katika Jamhuri ya Kidemkokrasia ya Kongo, mwanzoni mwa mwezi Septemba umesababisha vifo vya watu 42

https://p.dw.com/p/51P3r
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la afya Ulimwenguni WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus
WHO yasema mripuko wa Ebola ulisababisha vifo vya watu 42 DR KongoPicha: Fabrice Coffrini/AFP/Getty Images

WHO imesema watu wengine 64 walithibitishwa kuambukizwa ugonjwa huo, lakini ikasema kuwa hatari ya Ebola kuenea katika eneo hilo ni ndogo.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema shirika lake pamoja na washirika wake wanaendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya DRC za kuudhibiti ugonjwa huo.

Wiki mbili zilizopita wizara ya afya nchini Kongo ilianza kutoa chanjo dhidi ya Ebola.

Ugonjwa huo unaoambukizwa kupitia majimaji ya mwili umewauwa watu 15,000 barani Afrika ndani ya miongo mitano iliyopita.

Mripuko wa ugonjwa huo nchini Kongo kati ya mwaka 2018 na 2020 ulisababisha vifo vya takriban watu 2,300