1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Watu watatu wauawa katika miji ya Kherson na Donetsk

22 Machi 2024

Maafisa wa Ukraine wamesema watu watatu wamekufa katika miji ya Kherson na Donetsk kufuatia mashambulizi ya Urusi katika miji hiyo.

https://p.dw.com/p/4e05H
Athari ya uharibifu uliofanywa baada ya shambulio la Urusi katika viunga vya Odesa, kusini mwa Ukraine
Athari ya uharibifu uliofanywa baada ya shambulio la Urusi katika viunga vya Odesa, kusini mwa UkrainePicha: Nina Liashonok/Avalon/Photoshot/picture alliance

Mamlaka katika mji wa Kherson imeeleza kuwa, mwanamke mwenye umri wa miaka 70 alijeruhiwa vibaya kutokana na shambulio la Urusi na alifariki muda mfupi baadae akiwa njia kuelekea hospitali.

Na katika mji wa mashariki wa Donetsk, waendesha mashtaka wamesema vifo vya watu wawili vimetokea katika kitongoji kidogo cha Novohrodivka.

Soma pia: Urusi yarusha ndege 38 zisizokuwa na rubani Ukraine 

Watu wengine wawili pia wamejeruhiwa.

Urusi imekuwa ikishambulia maeneo mbalimbali ya Ukraine kwa zaidi ya miaka miwili sasa huku raia wa kawaida hasa wanaoishi karibu na uwanja wa mapmabano kati ya askari wa Ukraine na Urusi wakiuawa.