1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAfrika Kusini

Takriban watu 20 wafariki katika ajali Afrika Kusini

18 Septemba 2023

Ajali hiyo ya barabarani ilitokea Jumapili katika kijiji cha Musian kwenye mpaka na Zimbabwe.

https://p.dw.com/p/4WSek
Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi zenye viwango vya juu vya ajali za barabarani
Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi zenye viwango vya juu vya ajali za barabaraniPicha: Polícia da República de Moçambique

Takriban watu 20 wamefariki dunia katika ajali ya barabarani nchini Afrika Kusini. Ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Musian kwenye mpaka na Zimbabwe hapo jana. Watu hao walikuwa ni wafanyakazi wa kampuni kubwa ya madini ya "De Beers" inayohudumu nchini humo kwa zaidi ya miaka 30.       

Afisa wa usafiri katika jimbo la Limpopo, kaskazini mwa nchi hiyo, Vongani Chauke, amesema basi lililokuwa limewabeba wafanyakazi hao kutoka mgodi wa Venetia, mmoja wa migodi mikubwa ya almasi nchini humo, liligongana na lori Jumapili jioni na chanzo cha ajali hiyo hakijabainika wazi.

Mgodi wa Venetia, ambao uko karibu na mpaka wa Botswana na Zimbabwe, unachangia kwa mwaka zaidi ya asilimia 40 ya uzalishaji wa almasi nchini humo.

Afrika Kusini ina mojawapo ya miundo mbinu ya barabara iliyoendelea zaidi barani Afrika, lakini inaongoza pia kwa ajali za barabarani.