1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Afrika Kusini yajiandaa kwa mazishi ya Mwanamfalme wa Wazulu

16 Septemba 2023

Maelfu ya watu nchini Afrika Kusini wanakusanyika leo kutoa heshima za mwisho kwa mwanamfalme wa jamii ya Wazulu, Mangosuthu Buthelezi, aliyeaga dunia wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 95.

https://p.dw.com/p/4WPug
Mwanamfalme Mangosuthu Buthelezi
Mwanamfalme wa jamii ya Wazulu wa Afrika Kusini, Mangosuthu Buthelezi, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 95.Picha: Rajesh Jantilal/AFP/Getty Images

Tukio la kumwaga Mangosuthu linafanyika kwenye uwanja uliopo Ulundi, eneo ambalo lilikuwa mji mkuu wa zamani wa Ufalme wa Wazulu.

Rais Cyril Ramaphosa ni miongoni mwa wale watakaotoa hotuba ya salamu za rambirambi kabla ya mazishi ya kiongozi huyo aliyekuwa na wadhifa wa Waziri Mkuu wa Milki huru ya jamii ya Wazulu wa Afrika Kusini.

Kiongozi huyo wa jadi alikuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za Afrika Kusini lakini aliyehusishwa na wimbi la matukio ya kikatili enzi ya utawala wa wazungu wachache.

Anatuhumiwa kushirikiana na serikali ya makaburu wa Afrika Kusini kuhujumu harakati za chama cha ukombozi cha ANC za kumaliza enzi ya ubaguzi wa rangi mwanzoni mwa miaka ya 1990.