1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroNigeria

Wasichana 12 waliotekwa Nigeria waachiwa huru

Saleh Mwanamilongo
30 Novemba 2025

Kundi la wapiganaji wa itikadi kali za kiislamu lililowateka nyara wanawake na wasichana zaidi ya 300 kaskazini mashariki mwa Nigeria wiki moja iliyopita limewaachia huru wasichana 12 waliokuwa wamesalia.

https://p.dw.com/p/54W4S
Nigeria, Monguno 2025 | Askari wa Nigeria wa Kikosi cha Pamoja cha Kimataifa akifanya mazoezi
Nigeria ina historia ya utekaji nyara wa watu kwa wingi, mara nyingi ukifanywa na magenge ya wahalifuPicha: Joris Bolomey/AFP/Getty Images

Kundi la wapiganaji wa itikadi kali za kiislamu lililowateka nyara wanawake na wasichana zaidi ya 300 kaskazini mashariki mwa Nigeria wiki moja iliyopita limewaachia huru wasichana 12 waliokuwa wamesalia.

Abubakar Mazhinyi, mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Askira-Uba, katika jimbo la Borno, amesema waathirika wamepelekwa hospitali na hakuna kikomboleo kilicholipwa, kwani jeshi lilikuwa linawasaka watekaji.

Wanawake hao, wenye umri wa miaka 16 hadi 23, walitekwa karibu na mashamba yao katika eneo linalotumika kama maficho ya wanamgambo wa itikadi kali. Jimbo la Borno, kitovu cha mapigano kati ya jeshi na kundi la Boko Haram kwa miaka 16, bado linakabiliwa na vitisho kutoka makundi ya Boko Haram na ISWAP, licha ya kupungua kwa nguvu zao.

Mgogoro huo umesababisha vifo vya zaidi ya watu 40,000 na kuwahamisha zaidi ya milioni mbili, huku vitendo vya utekaji vikiongezeka nchini kote.