Watoto 50 kati ya 300 waliotekwa wawatoroka watekaji Nigeria
23 Novemba 2025
Matangazo
Kulingana na Chama cha Kikristo cha Nigeria, watoto hao waliotoroka kati ya Ijumaa na Jumamosi tayari wameungana na wazazi wao.
Zaidi ya wanafunzi 300 wenye umri kati ya miaka 8 na 18 na waalimu 12 walitekwa nyara na watu hao wasiojulikana hali inayowapa hofu raia wa taifa hilo.
Mamlaka zimesema vikosi maalumu vimeshaanza kufanya msako wa kujaribu kuwaokoa wanafunzi hao lakini haijataja idadi kamili ya waliotekwa.
Hili ni tukio la pili la aina hiyo ndani ya wiki moja baada ya wanafunzi wengine 25 kutekwa nyara katika jimbo la Kebbi.