1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waripablikani wanza safari ya kumpata Spika mpya Marekani

11 Oktoba 2023

Wabunge wa chama cha Republican katika bunge la wawakilishi Marekani watakutana kumchagua mmoja kati ya wagombea wawili kuongoza wingi wao mdogo bungeni.

https://p.dw.com/p/4XQ1I
Jengo la Bunge la Marekani
Jengo la Bunge la MarekaniPicha: Samuel Corum/Getty Images

Wabunge wa chama cha Republican katika bunge la wawakilishi Marekani watakutana leo kumchagua mmoja kati ya wagombea wawili Steve Scalise na Jim Jordan, kuongoza wingi wao mdogo bungeni, baada ya kundi dogo la wabunge wapinzani katika chama hicho kumuondoa spika Kevin McCarthy.

Huku wabunge hao wakikusanyika kwa ajili ya kura hiyo iliyofanywa faraghani, hakuna yeyote kati ya wagombea hao wawili Scalise na Jordan aliyeonekana kuwa na uwezekano wa kushinda moja kwa moja.

Soma pia:Spika wa Bunge la Marekani aanzisha uchunguzi wa kumshtaki rais Biden

Scalise anaungwa mkono na wabunge wengi wakongwe wa chama cha Republican naye Jordan ana uungwaji mkono wa wabunge wahafadhina wa chama hicho.

Kura hiyo ya faragha huenda ikawa mwanzo wa mchakato mrefu wa kumchagua spika mpya, baada ya kundi moja dogo la wabunge Warepublican kumuondoa McCarthy madarakani wiki iliyopita na kulemaza shughuli za bunge.