1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Warepublican wamteua Steve Scalise kuwania uspika

12 Oktoba 2023

Chama cha Republican kinachokabiliwa na mgawanyiko mkubwa kimemteua Steve Scalise kuchukua nafasi ya spika.

https://p.dw.com/p/4XT2B
Tangu kuondolewa kwa McCarthy, bado kunashuhudiwa mvutano miongoni mwa wabunge wa Republican.
Tangu kuondolewa kwa McCarthy, bado kunashuhudiwa mvutano miongoni mwa wabunge wa Republican.Picha: Win McNamee/AFP/Getty Images

Chama hicho kinapambana kuhakikisha kinaungana mara moja ili kumchagua mhafidhina huyo katika kura ya wazi.

Scalise anatarajiwa kujaza nafasi ya Kevin McCarthy aliyeondolewa.

Scalise, mbunge wa Louisiana, ambaye kwa sasa ni kiongozi wa walio wengi bungeni, alipata ushindi mwembamba katika kinyang'anyiro cha uteuzi dhidi ya Jim Jordan, ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya sheria ya bunge.

Scalise amewaambia Warepublican wenzake baada ya kuteuliwa kwamba wana kazi kubwa ya kufanya na kuongeza kuwa wanatakiwa kuhakikisha wanapeleka ujumbe kwa watu kote ulimwenguni kwamba bunge liko wazi  kwa ajili ya kuwatumikia watu.

Tangu kuondolewa kwa McCarthy wiki iliyopita, bado kunashuhudiwa mvutano miongoni mwa wabunge wa Republican.