1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAsia

Wanaharakati wa demokrasia wa Hong Kong watiwa hatiani

30 Mei 2024

Mahakama Kuu ya mji wa Hong Kong imewatia hatiani wanaharakati 14 wa demokrasia kwa kula njama za kufanya hujuma dhidi ya dola, ikiwa ni kesi kubwa ya kwanza chini ya sheria iliyoshinikizwa na watawala wa China.

https://p.dw.com/p/4gRx7
Hong Kong | Polisi wakilinda doria katika mahakama kuu.
Polisi wakiwa wanalinda doria katika Mahakama Kuu ya mjini Hong KongPicha: Tyrone Siu/REUTERS

Wale waliotiwa hatiani ni pamoja na wabunge wa zamani wanne ambao wanaweza kukabiliwa na hadi kifungo cha maisha jela pale mahakama itakapotoa hukumu wiki zinazokuja.

Wanasiasa wengine wawili wamefutiwa mashtaka kwenye kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka 2021 ikiwalenga wanaharakati 47 wa demokrasia.  

Soma pia:Wanaharakati wa demokrasia ya Hong Kong kuhukumiwa

Waendesha mashtaka waliwatuhumu wanaharakati hao kutaka kuiyumbisha serikali ya Hong Kong na kumwangusha kiongozi wa mji huo wenye utawala wa ndani kupitia kura isiyo rasmi waliyoiitisha.

Tangu kutungwa kwa sheria ya usalama ya Hong Kong mwaka 2020 chini ya shinikizo la serikali kuu ya China, wanaharakati wanasema haki na uhuru wa watu umebinywa na inatumika kuwaandama wapinzani.