1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Wanaharakati wa demokrasia ya Hong Kong kuhukumiwa

30 Mei 2024

Mahakama moja ya Hong Kong leo itaanza kutoa uamuzi katika kesi kubwa zaidi kufanyika katika eneo hilo dhidi ya wanaharakati wanaounga mkono demokrasia tangu China ilipoweka sheria ya usalama wa taifa

https://p.dw.com/p/4gR4z
Polisi wakabiliana na waandamanaji wanaopinga sheria ya usalama wa taifa, Hong Kong, iliyowekwa na serikali kuu ya China mnamo Julai 1, 2020
Polisi wakabiliana na waandamanaji wanaopinga sheria ya usalama wa taifa, Hong KongPicha: Deacon Lui/EyePress/Newscom/IMAGO

Majaji watatu wa mahakama kuu wanatarajiwa kuchukua hadi siku mbili kutoa uamuzi huo, huku washtakiwa 47 wakikabiliwa na kifungo cha maisha jela kwa tuhuma za njama ya kuhujumu mfumo wa serikali.

Soma pia:Sheria mpya ya usalama Hong Kong yaanza kutumika kuanzia leo

Washtakiwa 16 wakiwemo wanaharakati, wabunge wa zamani na madiwani wa wilaya wamepinga mashtaka hayo na hukumu dhidi yao itatolewa wiki hii.

Baadhi ya washtakiwa walikiri makosa

Washtakiwa wengine 31 walikiri makosa wakitarajia adhabu ndogo. Washtakiwa wengi wamezuiliwa gerezani tangu walipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mnamo Machi 2021.

Soma pia:China yawakemea wanaokosoa sheria ya usalama wa taifa ya Hong Kong

Eric Lai, mtafiti katika Kituo cha Sheria za Asia cha Chuo Kikuu cha Georgetown, amesema uamuzi wa leo utaonyesha ikiwa Hong Konginachukulia ushiriki wa kisiasa usio na vurugu kuwa uhalifu.