1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabunge Hong Kong wapitisha sheria mpya ya usalama

19 Machi 2024

Wabunge wa Hong-Kong wamepitisha kwa kauli moja sheria mpya ya usalama wa taifa, iliyopendekezwa na kiongozi John Lee na ambayo inaipatia serikali uwezo wa kuukandamiza upinzani.

https://p.dw.com/p/4duK6
China | Hongkong
Bunge la Hong KongPicha: Vernon Yuen/NurPhoto/picture alliance

Wabunge wa mji wenye mamlaka ya ndani wa Hong-Kong wamepitisha kwa kauli moja sheria mpya ya usalama wa taifa, iliyopendekezwa na kiongozi John Lee na ambayo inaipatia serikali ya mji huo uwezo mkubwa wa kuukandamiza upinzani. Muswada huo ulianzishwa Machi 8 mwaka huu.Mkuu wa zamani wa usalama kuchaguliwa kiongozi Hong Kong

Sheria hiyo inalenga kutoa adhabu kali kwa vitendo mbalimbali ambavyo mamlaka itaamua kuwa vinatoa kitisho kwa usalama wa taifa, huku makosa makubwa zaidi, ikiwa ni pamoja na uhaini na uchochezi wa uasi, ambavyo vinaweza kuadhibiwa kwa kifungo cha maisha jela.

Hii ni hatua ya hivi punde dhidi ya upinzani wa Hong-Kong kufuatia maandamano ya mwaka 2019 ya kuunga mkono demokrasia na imeshabihiana na sheria iliyochukuliwa miaka minne iliyopita huko China na ambayo kwa kiasi kikubwa imekandamiza upinzani.