1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani kuzuia visa za maafisa kadhaa wa Hong Kong

Sylvia Mwehozi
30 Machi 2024

Marekani imetangaza kuwa itawawekea vizuizi vipya vya viza maafisa wa Hong Kong wanaohusika na ukandamizaji wa haki katika mji huo ambao ni sehemu ya China.

https://p.dw.com/p/4eHJH
Antony Blinken
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken Picha: Saul Loeb/AP/picture alliance

Marekani imetangaza kuwa itawawekea vizuizi vipya vya viza maafisa wa Hong Kong wanaohusika na ukandamizaji wa haki katika mji huo ambao ni sehemu ya China, siku chache baada ya sheria mpya ya usalama wa taifa kuanza kutumika.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alisema katika taarifa yake kwamba Beijing imeendelea kuchukua hatua za kiwango cha juu dhidi ya uhuru wa mji huo, taasisi za kidemokrasia, haki na uhuru kwa mwaka uliopita.

Blinken ameeleza kuwa ili kukabiliana na kuongezeka kwa ukandamizaj na vikwazo dhidi ya vyama vya kiraia, vyombo vya habari, na sautiChina yawakemea wanaokosoa sheria ya usalama wa taifa ya Hong Kong za upinzani, wizara ya mambo ya nje inachukua hatua za vizuzi vipya vya viza kwa maafisa kadhaa wa Hong Kong. China yawakemea wanaokosoa sheria ya usalama wa taifa ya Hong Kong

Hata hivyo hakutoa maelezo ya kina juu ya hatua hizo za viza ama maafisa watakaolengwa.