1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiTunisia

Tunisia: Wahamiaji wa Kiafrika bado wakabiliwa na hali ngumu

Saumu Mwasimba
24 Machi 2023

Baada ya kuaandamwa kwa wahamiaji nchini Tunisia na kusababisha wengi kuondoka kwa maboti ya wasafirishaji watu kwa magendo kuelekea nchini Italia, raia wa nchi za Kiafrika bado wamebakia hawana makaazi wala ajira.

https://p.dw.com/p/4PDmq
Tunesien gestrandete Flüchtlinge aus Subsahara Afrika
Picha: Jihed Abidellaoui/REUTERS

Mnamo wiki hii wahamiaji kadhaa wa kiafrika waliandamana nje ya ofisi ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi mjini Tunis.

Wahamiaji hao wakiwemo watoto wamekuwa wakiishi katika kambi ya muda tangu mamlaka za Tunisia zilipowataka wamiliki wa majumba kuwatimua kwa nguvu waafrika weusi. Baadhi ya raia hao wanasema bado wanakabiliwa na mashambulizi ya kibaguzi.

Soma pia: Mamia ya wahamiaji wa Kiafrika wenye hofu waikimbia Tunisia

Jana Alhamisi, naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Barbara Leaf, aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba kauli ya rais wa Tunisia kuhusu wahamiaji wakiafrika imeanzisha mashambulizi na wimbi la mitizamo ya chuki nchini humo,huku mashirika ya haki za binadamu yakisema mamia ya wahamiaji wameripoti kushambuliwa na kunyanyaswa.