Waasi wa M23 waimarisha udhibiti wa mji wa Uvira
11 Desemba 2025
Mashuhuda wameripoti milio ya risasi pembezoni mwa mji huo, huku wakazi wakijitokeza kutafuta chakula baada ya siku ya iliyojaa hofu na kukimbia makazi yao.
Serikali ya Kinshasa imeonya kuwa mashambulizi yanayodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, yanaweza kuvuruga makubaliano ya amani yaliyosimamiwa Washington wiki iliyopita.
Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya watu 200,000 wamekimbia katika siku chache, na karibu 25,000 wamevuka mpaka kuingia Burundi.
Mashirika ya misaada yamesitisha shughuli maeneo ya Kivu Kusini, na shule zaidi ya 30 zimegeuzwa makazi ya wakimbizi, hatua inayoongeza hatari ya milipuko ya magonjwa. Waangalizi wa kimataifa wanasema kutengwa kwa M23 kwenye mazungumzo ya amani kunafanya suluhu ya kudumu ionekane mbali.