1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUbelgiji

Von der Leyen akutana na Guterres mjini Brussels

20 Machi 2024

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amekutana kwa mazungumzo hii leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

https://p.dw.com/p/4dwiW
Brüssel | Ursula von der Leyen | Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der LeyenPicha: Kenzo Tribouillard/dpa/Pool AFP/AP/picture alliance

Viongozi hao wawili walijadiliana kuhusu migogoro mbalimbali inayoendelea duniani. Akimpokea mjini Brussels nchini Ubelgiji, Von der Leyen amesema,

"Leo hii mpendwa Antonio, ninafuraha mno kukuona hapa Brussels, wakati ambapo tunakabiliwa na migogoro kadhaa ambayo ni tete, inayoshabihiana na ya kimataifa. Iwe mzozo wa Ukraine au Gaza, Sudan au Haiti, hii inasisitiza kuwa ushirikiano kati ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa ni muhimu zaidi kuliko wakati wowote ule. Tunafanya kazi pamoja kusaidia kurejesha amani na utulivu katika maeneo yenye machafuko," alisema Von der Leyen.

Rais huyo wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya amesema kuna haja ya kufanya mabadiliko kwenye taasisi za kimataifa kwani mifumo iliyopo kwa sasa haiwezi kukabiliana ipasavyo na changamoto hizo.