1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Ulaya wakutana kujadili msaada kwa Ukraine

Sylvia Mwehozi
15 Machi 2024

Viongozi wa Ujerumani, Ufaransa na Poland wamekutana mjini Berlin kujadili uungwaji mkono zaidi kwa Ukraine, wakati Urusi ikipiga kura katika uchaguzi unaotarajiwa kurefusha muda wa Rais Vladimir Putin mamlakani.

https://p.dw.com/p/4dgEb
Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Fred Dugit/dpa/picture alliance

Mkutano huo ni ishara ya kuonyesha umoja na mshikamano wakati Kyiv ikikabiliana na upungufu wa rasilimali za kijeshi, huku pia Urusi ikipiga kura katika uchaguzi unaotarajiwa kurefusha muda wa Rais Vladimir Putin mamlakani.

Scholz kukutana na Macron na Tusk mjini Berlin kujadili sera za Ukraine

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amewakaribisha rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk, katika mkutano wa kilele wa ushirika wa mataifa hayo matatu unaofahamika kama Weimar Triangle.

Kansela Scholz amesema kuwa vikosi vya Ukraine vina matumaini ya kupatiwa  msaada zaidi wa kijeshi kutoka kwa washirika wake wa nchi za magharibi.