Vijana waviijia juu vyama vyao vya CDU na SPD | Matukio ya Kisiasa | DW | 09.02.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Ujerumani

Vijana waviijia juu vyama vyao vya CDU na SPD

Vijana wa chama cha CDU wanataka chama hicho kijiunde upya na kuanza kumjenga mrithi wa kiongozi wake kansela Angela Merkel na tawi la vijana wa SPD wao wanasema hawataki muungano wa vyama.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel huku akiwa anatazamia kuiweka serikali mpya kazini kumaliza mkwamo wa kisiasa wa  zaidi ya miezi minne katika nchi yenye uchumi mkubwa barani Ulaya. Bibi Merkel aliridhia muafaka na kukubali kuipoteza wadhfa wa wizara yenye nguvu ya Fedha ambaye wakati wote ilikuwa anashikiliwa na waziri anayetoka kwenye chama cha kihafidhina. Kansela Merkel ameyakubali hayo kwa ajili ya kufikiwa makubaliano na chama cha Social Demokratic, (SPD) lakini ni hatua ambayo imewakasirisha wengi katika chama chake.

Kiongozi wa tawi la vijana wa vyama vya CDU/CSU Paul Ziemiak (DW)

Kiongozi wa tawi la vijana wa vyama vya CDU/CSU Paul Ziemiak

Paul Ziemiak, kiongozi wa tawi la vijana wa chama cha Christian Democratic Union (CDU) na chama ndugu cha (CSU) ambavyo kwa pamoja vinaunda vyama vya Kihafidhina amesema chama hicho kinahitajika kufikiria juu ya nani atakayechukua nafasi ya Merkel ambaye muhula wake wa nne uko ukingoni kumalizika.

Ziemiak aliliambia shirika la utangazaji la Ujerumani Deutschlandfunk kwamba ikiwa chama cha CDU hakijiandai kubadilika ili kupata sura mpya basi hakika hali itaweza kuwa mbaya sana. Amesema vijana wanataka kuwaona wanasiasa vijana wanakuwa sehemu ya serikali na pia kuwemo katika nyadhfa kadhaa za uongozi wala hawana tena muda zaidi wa kusubiri. Tawi hilo la vijana lina wanachama karibu 115,000 ambalo ni tawi kubwa kabisa la kisiasa la vijana barani Ulaya, lakini ushawishi wake ndani ya chama hauna kifani.

Kansela Angela Merkel na Kiongozi wa tawi la vijana wa vyama vya CDU/CSU Paul Ziemiak (picture-alliance/dpa/M. Kappeler)

Kansela Angela Merkel na Kiongozi wa tawi la vijana wa vyama vya CDU/CSU Paul Ziemiak

Ziemiak amesema Kansela Merkel anahitaji kufafanua jinsi nafasi za kazi zitakavyogawanywa katika serikali na katika chama siku za baadaye. Hayo atahitaji kuyafafanua wakati wa mkutano wa chama cha CDU utakaofanyika tarehe 26 mwezi huu wa Februari.

Kutoridhika kumetawala ndani ya chama hicho cha CDU miongoni mwa wanachama walio kwenye ngazi ya chini ambao wengi wanadhani chama chao kilishindwa kujadili vizuri katika mazungumzo ya kuunda serikali na chama cha SPD

Kiongozi wa tawi la vijana wa chama cha SPD Kevin Kevin Kühnert (picture-alliance/dpa/K.D. Gabbert)

Kiongozi wa tawi la vijana wa chama cha SPD Kevin Kevin Kühnert

Wakati huo huo, wanachama 464,000 wa chama cha SPD bado wana haki ya kupinga kuundwa kwa muungano huo mkubwa baina ya chama chao cha SPD na vyama vya kihafidhina vya CDU na CSU katika kura inayosubiriwa ambayo itapigwa kwa njia ya posta na matokeo yake yatatangazwa mnamo tarehe 4 mwezi ujao wa Machi.

Kevin Kuehnert kiongozi wa tawi la vijana wa chama hicho cha SPD anazunguka nchi nzima kuwashawishi vijana waukatae muungano huo mkubwa.

Mwandishi: Zainab Aziz/RTRE

Mhariri: Grace Patricia Kabogo

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com