1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki-Syria: Idadi ya vifo yaongezeka na kufikia 28,000

12 Februari 2023

Idadi ya vifo kutokana na mitetemeko ya ardhi nchini Uturuki na Syria sasa imefikia zaidi ya watu 28,000. Vifo 24,517 vimeripotiwa Uturuki huku 3,574 vikiripotiwa kutoka Syria.

https://p.dw.com/p/4NNqD
Türkei, Antakya | Erdbeben
Picha: Bernat Armangue/AP/picture alliance

Shirika la utangazaji la serikali ya Uturuki  TRT, limetangaza leo kuwa mtoto wa miezi 7 ameokolewa akiwa hai kusini-mashariki katika jimbo la Hatay baada ya kukaa masaa 140 chini ya vifusi.

Mtaalamu wa Ujerumani na mfanyakazi wa shirika la misaada la NAVIS Thomas Geiner, ameonya juu ya hatari ya kutokea milipuko ya magonjwa kutokana na uhaba wa maji safi na miundombinu muhimu kama choo huku akitoa wito wa kupatikana misaada kwa haraka.