1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Urusi yawahamisha watoto 5,000 kutoka mkoa wa Belgorod

Sylvia Mwehozi
30 Machi 2024

Urusi imewahamisha watoto wapatao 5,000 kutoka mkoa wa Belgorod unaopakana na Ukraine kufuatia wiki kadhaa za mashambulizi makali ya Kyiv.

https://p.dw.com/p/4eGtA
Mtoto katika mkoa wa Belgorod
Urusi ikiwasajili watoto wanaohamishwa mkoa wa Belgorod Picha: Mikhail Tokmakov/TASS/dpa/picture alliance

Urusi imewahamisha watoto wapatao 5,000 kutoka mkoa wa Belgorod unaopakana na Ukraine kufuatia wiki kadhaa za mashambulizi makali ya Kyiv. Mamlaka za mkoa huo zinasema wiki iliyopita pia watato wengine 9,000 walihamishiwa kwenye mikoa mingine baada ya wimbi la mashambulizi ya mabomu ya kuvuka mpaka na droni yaliyowaua watu 12.

Mkoa huo wa Belgorod umekuwa ukilengwa mara kwa mara na kile maafisa wa Urusi wanachokitaja kuwa ni mashambulizi ya kiholela ya Ukraine tangu mzozo huo uanze zaidi ya miaka miwili iliyopita. Siku ya Ijumaa, ndege isiyo na rubani ya Ukraine ilianguka katika jengo la ghorofa katika mkoa huo na kumuua mwanamume mmoja na kuwajeruhi wengine wawili, akiwemo mkewe.