1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yatangaza kuondoa majeshi yake katika eneo la Kharkiv

Sudi Mnette
10 Septemba 2022

Wakati Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy akisema jeshi la taifa lake limefanikiwa kulikomboa eneo la kilometa za mraba 2,000.Urusi imetangaza kuyaondoa majeshi yake mashariki mwa Kharkiv.

https://p.dw.com/p/4GgHA
Ukraine Charkiw | Ukrainische Soldaten auf gepanzertem Fahrzeug
Picha: Juan Barreto/AFP

Katika taarifa yake kwa njia ya video Zelensky amesema hatua ya kulikomboa eneo hilo inatokana na kufanikiwa kwa operesheni yake ya kukabiliana na vikosi vya Urusi ambayo iliüanza mapema mwezi huu.

Awali Ijumaa Rais Zelensky alisema vikosi vyake vimeweza kuyadhibiti maeneo ya makazi zaidi ya 30 katika mkuo huo wa Kharkiv.

Urusi imejiondoa katika maeno mawili ya kimkakati ya Kharkiv

Ukraine I St. Nikolaus-Kathedrale in Kupiansk
Kanisa la Mtakatifu Nicholas la Kupiansk, KharkivPicha: RIA Novosti/SNA/IMAGO

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imetangaza kuyaondoa majeshi yake katika maeneo mawaili ya mashariki mwa Ukarine katika mkoa wa Kharkiv, eneo ambalo vikosi vya Ukraine vimekuwa vikipiga hatua muhimu ya kusonga mbele katika makabiliano yake na Urusi tangu juma lililopita.

Taarifa hizo zinatolewa baada ya siku kadhaa ya kusonga mbele kwa vikosi vya Ukraine kwa upande wa kusini wa Kharkiv, katika mji huo ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine, katika kile kinachotazamwa kama mafanikio makubwa katika uwanja wa vita, tangu vilipozuia jaribio la Urusi kuuteka mji mkuu wa Kyiv, mwanzoni kabisa mwa vita viliyodumu karibu miezi saba sasa.

Urusi yaeleza sababu ya kujiondoa katika maeneo hayo

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi wa Ukraine amesema Igor Konashenkov amsema vikosi vya Urusi vinarejea kwenda kujipanga upya katika eneo la Balakliya na Izyum, huko mashariki mwa mkoa wa Donetsk.

The Wider Image: Ukraine firefighters adapt to working in war zone
Kikosi cha kuzima moto cha Ukraine mjini KharkivPicha: Leah Millis/Reuters

Izyum ilikuwa kambi kubwa ya vikosi vya Urusi katika mkoa wa Kharkiv, na mapema wiki hii vidio za katika mitandao ya kijamii zilionesha wakazi wa Balaklia waonesha furaha na kuwashangilia wanajeshi wa Ukraine waliokuwa wakiingia katika viunga vya mji huo.

Msemaji Konashenkov hatua ya Urusi imetokana na mpango wa kufanikisha malengo kadhaa, katika opereesheni maalumu ya kijeshi yenye lengo la kuikomboa Donbas, mmoja kati ya mikoa ya Ukraine ambayo Urusi imeitangaza kuwa huru.

Sababu ya kujiondoa ili kutoa zingatio kwa eneo la  Donetsk ni sawa na ile iliyoipa uhalali Urusi katika hatua ya kuyarejesha nyuma majeshi yake kutoka katika maeneo ya karibu na Kyiv, mwanzoni mwa mwaka huu pale iliposhindwa kuudhibiti mji mkuu huo.

Uingereza imesema Ukraine imesonga mbele kwa kilomita 50

Awali Jumamosi Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema kwamba inaamini

Wanajeshi wa Ukraine wamesonga mbele hadi kilomita 50 kusini mwa Kharkiv, na kuvisukuma  vikosi vya Urusi karibu na eneo la Izyum. Taarifa inasema kilichjitokeza kimevistusha vikosi vya Urusi.

Soma zaidiMarekani kutoa msaada wa dola bilioni 2 kwa Ukraine

Licha ya mafanikio ya Ukraine, Ijumaa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO walionya kwamba vita hivyo vinaweza kuendelea kwa miezi. Blinken alisema mzozo huo unaingia katika kipindi kigumu na hivyo kuwataka waungaji mkono wa Ukraine akimaanisha mataifa ya Magharibi wa Ukraine kuendelea kuiunga mkono hata katika kile alichokiita kipindi kigumu cha msimu wa baridi.

Chanzo: AP/RTR