1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaiteka miji miwili midogo ya Kusini mwa Ukraine

Saumu Mwasimba
28 Februari 2022

Urusi na Ukraine zatarajiwa kuanza mazungumzo huko mpakani mwa Belarus lakini rais Zelensky hana imani na mkutano huo

https://p.dw.com/p/47i1E
Ukraine I gepanzerter Mannschaftstransportwagen brennt  nach Kämpfen in Charkiw
Picha: Marienko Andrew/AP/picture alliance

Hali bado ni ya taharuki kwa Waukraine wanaoendelea kuikimbia nchi yao kufuatia uvamizi wa Urusi. Wanajeshi wa Urusi wameshaiteka miji miwili midogo huko Kusini Mashariki mwa Ukraine na eneo linalozunguka kinu cha Nuklia. Saumu Mwasimba anaarifu yaliyojiri mpaka wakati huu,ndani ya Ukraine na upande wa Urusi.

Soma pia: WBaraza kuu la Umoja wa Mataifa kujadili Ukraine kwa dharura

Vikosi vya ardhini vya Urusi vilijaribu kuidhibiti miji mikubwa kadhaa mengine lakini na walikabiliwa na upinzani mkali wa Ukraine. Aidha  bado taharuki inaendelea kuwakabili wananchi wa Ukraine ambapo Umoja wa Mataifa umesema tayari zaidi ya watu laki tatu na sitini elfu  wameshaikimbia nchi. Bado maelfu ya watu wanaendelea kuikimbia nchi kutafuta usalama:

" Nilichukua Treni kutoka Lviv kufika hapa ilikuwa ngumu sana watu walikuwa wengi,ilikuwa inatisha na hatari sana kimwili na kiakili. Watu wako kwenye taharuki kubwa,watu

Polen ukrainische Flüchtlinge an der Grenze
Watu 213,000 wamekimbilia Poland kutoka UkrainePicha: Omar Marques/Getty Images

wamechanganyikiwa na watu wakiwa kwenye khofu wanabadilika wanakuwa wabinafsi na kusahau kila kitu.

Hali hiyo inawakabili watu wengi wanaoikimbia Ukraine kwa hivi sasa wakielekea nchi jirani ya Poland,Romania na kwengineko. Rais Vladmir Putin jana Jumapili aliyaweka kikosi chake kinachohusika na sialaha za Nyuklia katika tahadhari kubwa  katika wakati ambapo nchi za Magharibi zikionekana kujiandaa kupinga mashambulizi ya nchi hiyo dhidi ya Ukraine. Ingawa pia hii leo Jumatatu Urusi na Ukraine zinajiandaa kuanza kwa mara ya kwanza mazungumzo ya kutafuta mwafaka wa kumaliza vita hii,tangu Urusi ilipoivamia Ukraine. jana Ukraine ilisema imekubali kupeleka ujumbe wake kukutana na wawakilishi wa Urusi katika eneo la mpaka na Belarus.

Soma pia: Putin aamuru vikosi vya kujilinda viwe kwenye tahadhari

Leo Jumatatu Belarus iliripoti kwamba tayari eneo la mkutano limeshaandaliwa na mazungumzo yataanza mara moja pindi zitakapofika pande zote mbili.

Lakini kutokana na serikali ya Ukraine kuripoti vifo vya mamia ya wananchi wake na hatua ya Urusi kuiteka miji kadhaa muhimu,rais Volodymr Zelensky amesema anamashaka kuhusu mazungumzo hayo     ,amsema haamini ikiwa kweli yataleta matokeo yoyote ingawa wako tayari kujaribu kuzungumza.

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri: Daniel Gakuba