1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaishambulia tena Kyiv kwa makombora

7 Februari 2024

Urusi imefanya mashambulizi kadhaa ya makombora mjini Kyiv asubuhi ya Jumatano yaliyojewaruhi watu wawili na kusababisha kukatika kwa umeme katika baadhi ya sehemu katika huo mji mkuu wa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4c7bO
Vitali Klitschko - Kyiv - Ukraine
Meya wa Kyiv, Vitali Klitschko, anasema mifumo ya ulinzi iliyadunguwa baadhi ya makombora ya Urusi kuelekea mji huo.Picha: Ukrinform/dpa/picture alliance

Kulingana na ujumbe wa meya wa mji wa Kyiv, Vitali Klitschko, katika mtandao wa Telegram, mifumo ya ulinzi wa angani imeharibu baadhi ya makombora hayo.

Haya yanafanyika wakati ambapo mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), Rafael Grossi, akiwa amesafiri kuelekea Ukraine, kutazama hali ilivyo katika kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhya kilichotekwa na Urusi.

Soma zaidi:Ukraine yakataa wito wa Urusi kwa Mariupol kujisalimisha 

Akizungumza na waandishi wa habari, Grossi, alisema mfumo wa usambazaji wa maji ya kukipoza kinu hicho uliathirika kufuatia uharibifu uliofanywa katika Bwawa la Kakhovka.