Migogoro
Urusi, Ukraine zaendelea kushambuliana
27 Novemba 2025
Matangazo
Urusi pia imesema wanajeshi wake wamefanya mashambulizi yaliyoilenga miundombinu ya nishati na uchukuzi nchini Ukraine, wakati Ukraine imejibu kwa kukishambulia kiwanda cha Urusi cha kutengeneza silaha.
Mpango wa amani wa Trump wakosolewa
Mashambulizi ya pande hizo mbili yanajiri wakati wabunge kadhaa wa chama cha Republican wamekosoa vikali namna Rais Donald Trump anavyoushughulikia mpango uliopendekezwa wa kurejesha amani Ukraine.
Wabunge hao wamesema mpango huo wenye vipengele 28 unaipendelea Urusi. Hofu hiyo imechochewa na ripoti ya shirika la habari la Bloomberg iliyovujisha mazungumzo ya siri Jumanne kati ya mwakilishi wa Trump Steve Witkoff na msaidizi wa Rais wa Urusi Vladimir Putin, Yuri Ushakov yaliyoashiria kuipendelea Urusi.