1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu kadhaa wameuwawa katika mashambulizi ya Urusi

Sylvia Mwehozi
15 Machi 2024

Urusi na Ukraine zimedai kwamba mashambulizi ya usiku kucha kutoka kila upande yamewaua raia, wakati ambapo mataifa hayo yakianzisha wimbi la mashambulizi ya angani na droni.

https://p.dw.com/p/4dgIR
Ukaine |
Mashambulizi zaidi yafanyika Ukraine Picha: Viacheslav Ratynskyi/REUTERS

Kyiv imesema shambulio la droni la Urusi limewaua watu wawili katika mkoa wa katikati mwa Ukraine wa Vinnytsia, huku shambulio la makombora kwenye mkoa wa Zaporizhzhia likisababisha kifo cha mwanamke mmoja. 

Mkuu wa jeshi la Ukraine Oleksandr Syrsky anadai Urusi ilianzisha wimbi la mashambulizi kujaribu kusonga mbele zaidi katika eneo hilo.

Umoja wa Ulaya waonya juu ya mustakabali wa vita vya Ukraine

Maafisa wa Urusi nao wameripoti makombora ya Ukraine katika mji wanaoudhibiti wa Donetsk, kuwa yamewaua watoto watatu. 

Mashambulizi mengine ya makombora ya Ukraine yameripotiwa katika mkoa wa mpakani wa Belgorod na kusababisha kifo cha afisa mmoja upande wa Urusi.