1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNCTAD - itachukua miongo uchumi Palestina kuimarika

25 Novemba 2025

Vita vya miaka miwili huko Gaza na vikwazo vya kiuchumi vimesababisha kuporomoka pakubwa kwa uchumi wa Palestina na kuondoa juhudi za miongo kadhaa za kuimarika kwake.

https://p.dw.com/p/54DzU
Westjordanland Nablus 2025 | Israelische Soldaten bei Razzia nach Anstieg der Gewalt seit Gaza-Krieg
Picha: Zain Jaafar/AFP/Getty Images

Kulingana na ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo, UNCTAD, iliyotolewa na Katibu Mkuu wa shirika hilo Pedro Moreno, kufikia mwishoni mwa mwaka jana huko Palestina, Pato Jumla lilishuka na kufikia kiwango kile cha mwaka 2003.

"Ripoti yetu inatoa mwito wa mpango mpana wa kuufufua uchumi wa Palestina. Mpango huu unajumuisha ushirikishwaji wa msaada ya wa kimataifa, kurejeshwa kwa miamala ya usambazwaji wa fedha na serikali na hatua za kurahisisha biashara na uwekezaji."

Ripoti hiyo inasema kiwango cha uharibifu uliofanywa Gaza baada ya vita vya Israel dhidi ya wanamgambo wa Hamas, kinamaanisha Palestina itategemea pakubwa msaada wa kimataifa na kuimarika kwa uchumi wake kutachukua miongo kadhaa.

Wakati huo huo Shirika la Haki la Umoja wa Mataifa limesema raia 127 wameuwawa huko Lebanon kwa mashambulizi ya jeshi la Israel tangu usitishwaji wa mapigano utangazwe yapata mwaka mmoja uliopita.

Shirika hilo limetoa wito wa uchunguzi kufanyika na usitishwaji huo wa mapigano kuheshimiwa.