1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya warefusha muda wa vikwazo kwa Sudan

22 Septemba 2025

Umoja wa Ulaya umetangaza hatua za kurefusha vikwazo kwa wote wanaohusika na vita vya nchini Sudan. Vikwazo hivyo vimerefushwa kwa mwaka mmoja zaidi hadi ifikapo mwezi Oktoba mwaka ujao wa 2026.

https://p.dw.com/p/50u3U
Sudan inakabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe
Khartoum, SudanPicha: AFP

Vikwazo vilivyorefushwa ni pamoja na kutaifishwa mali za wanaohusika na mgogoro wa Sudan na kunyimwa ruhusa ya kuzitembelea nchi za Umoja wa Ulaya.

Wanaohusika na vikwazo hivyo ni watu kumi na mashirika manane pamoja na kampuni zinazojihusisha na utengenezaji wa silaha na magari ya jeshi la Sudan linaloongozwa na jenerali Abdel-Fattah al-Burhan.

Vikwazo hivyo pia ni kwa kampuni nyingine tatu zinazohusika na ununuaji wa vifaa vya kijeshi kwa ajili ya vikosi vya RSF vinavyoongozwa na Mohamed Hamdan Daglo.