Ulaya yaibwaga Marekani katika Kombe la Ryder | Michezo | DW | 30.09.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Ulaya yaibwaga Marekani katika Kombe la Ryder

Timu ya bara la Ulaya ya mchezo wa golf imepata ushindi kwa mara nyingine tena katika kombe maarufu duniani la Ryder. Ulaya iliishinda Marekani katika mashindnao hayo.

Ushindi wa timu ya bara la Ulaya dhidi ya Marekani mjini Gleneagles ulikuwa wa kuumiza sana , hususan baada ya matamshi ya Phil Mickelson mchezaji wa timu ya Marekani mwenye uzoefu mkubwa zaidi dhidi ya mchezaji mwenzake Tom Watson.

Ikilinganishwa na wachezaji wa timu ya Ulaya ambayo ina wachezaji kutoka Uingereza, Wales , Scotland , Ireland ya kaskazini, Uhispania, Ufaransa, Ujerumani , Sweden, Denmark na Ufaransa walikuwa na lengo moja tu la ushindi na kuwa pamoja wakiunganishwa na nahodha wao , Paul McGinley.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / dpae / rtre , ZR
Mhariri: Iddi Ssessanga