1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yakabiliana na mashambulizi ya Urusi huko Avdiivka

21 Oktoba 2023

Rais Volodymyr Zelenskiy amesema vikosi vya Ukraine vimekabiliana na mashambulizi mapya ya Urusi kwenye mji wa mashariki wa Avdiivka.

https://p.dw.com/p/4Xq7h
Ukraine Avdeevka Soldat Ruinen
Picha: Ozge Elif Kizil/Anadolu/picture alliance

Rais Volodymyr Zelenskiy amesema vikosi vya Ukraine vimekabiliana na mashambulizi mapya ya Urusi kwenye mji wa mashariki wa Avdiivka.

Zelenskiy na makamanda wakuu wa kijeshi wa Ukraine wametembelea eneo la kusini la Kherson, na kufanya tathmini katika mji huo na miji ya Avdiivka na Kupiansk, ambako wanajeshi wa Urusi wamezidisha mashambulizi. Hapo awali, wizara ya ulinzi ya Urusi ilidai kuwa imeharibu baadhi ya magari ya kijeshi ya Ukraine karibu na mji wa Avdiivka.

Vikosi vya Ukraine vimekuwa vikipiga hatua za kusuasua katika mashambulizi yake iliyoyaanzisha mwezi juni dhidi ya mashambulizi makali ya Urusi katika maeneo ya mashariki na kusini. Mji wa Avdiivka uko kilomita 15 kaskazini mwa Donetsk na umekuwa ishara ya upinzani ya Ukraine tangu uvamizi wa kwanza mnamo mwaka 2014.