1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Ujumbe wa UM wasema hautoondoka mji wa Akobo, Sudan Kusini

10 Machi 2026

Ujumbe wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini umesema hautatekeleza amri ya serikali ya nchi hiyo ya kuifunga kambi yake kwenye mji wa Akobo unaokabiliwa na kitisho cha mapigano.

https://p.dw.com/p/5A7UK
Sudan Kusini Akobo 2026 | Upinzani
Mji wa Akobo nchini Sudan Kusini umo kwenye kitisho cha mapigano kati ya serikali na upinzani. Picha: Luis Tato/AFP

Mkuu wa ujumbe huo, Anita Kiki Gbeho amesema wanafanya mawasiliano na upande wa serikali kuu, ile ya jimbo na washikadau wengine kuhusiana na amri hiyo ambayo amesema hawataitii na wataendelea kubakia kwenye mji huo ili kuwalinda raia.

Vikosi vya serikali ya Rais Salva Kiir vinataka kufanya mashambulizi kwenye mji huo ili kuukamata kutoka mikononi mwa wapiganaji wa upinzani wanaomtii aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar.

Duru kutoka mji huo ulio kwenye mpaka na Ethiopia zinasema, maelfu ya watu wameukimbia tangu serikali ilipotoa amri ya kuwataka kuuhama.