Uhispania baada ya Uchaguzi wa Bunge | Matukio ya Kisiasa | DW | 29.04.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Uhispania baada ya Uchaguzi wa Bunge

Kizungumkuti kiko vile vile kama kilivyokuwa kabla ya uchaguzi wa bunge kuitishwa nchini Uhusipiakuti.Waziri mkuu Pedro Sanachez atakuwa na kishindo kikubwa kusaka washirika kuunda serikali

Waziri mkuu wa Uhispania, msoshalisti Pedro Sanchez, ameibuka na ushindi wa uchaguzi wa bunge. Lakini kutokana na kutopata ushindi  mkubwa wa kutosha, itabidi atafute washirika kuweza kuunda serikali katika nchi iliyogawika ambako chama cha siasa kali za mrengo wa kulia kitawakilishwa kwa mara ya kwanza bungeni, miaka 40 baada ya kumalizika utawala wa kiimla wa  Francisco Franco. 

Uchaguzi huo wa jana unaweza kuendeleza hali ya vurugu inayogubika mandhari ya kisiasa nchini Uhispania tangu mfumo wa vyama viwili vya kisiasa-wahafidhina na wasoshaliti ulipomalizika mwaka 2015, na bunge kudhoofika huku nchi ikikabwa na jaribio la kutaka kujitenga jimbo la Catalonia mwajka 2017.

Wafuasi wa chama cha kisoshalisti PSOE wanasherehekea ushindi mjini Madrid

Wafuasi wa chama cha kisoshalisti PSOE wanasherehekea ushindi mjini Madrid

Kishindo cha kuunda serkali

Baada ya kuhesabiwa asili mia 99 ya kura chama cha kisoshalisti cha waziri mkuu Pedro Sanchez kimejipatia asili mia 29 ya kura na wabunge 123. Amejipatia viti  40 zaidi ikilinganishwa na uchaguzi wa  mwaka 2016-yuko mbali lakini ya viti 176 vinavyohitajika kuweza kuunda serikali katika bunge hilo lenye viti 350. Hata wasoshalisti wakiunda serikali ya muungano pamoja na wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kushoto "Unidas Podemos" watahitaji viti 10 zaidi kuweza kudhibiti wingi mkubwa bungeni. Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 47 amewatolea wito waaasiasa wote washirikiane kuunda serikali inayoelemea upande wa Umoja wa Ulaya. Anasema sharti pekee la kushiriki serikalini ni kuheshimu katiba na kuimarisha maisha ya jamii."

Mwenyekiti wa chama cha kihafidhina cha PP, Pablo Casado

Mwenyekiti wa chama cha kihafidhina cha PP, Pablo Casado

Vyama vya mrengo wa kulia vimepwaya licha ya Vox kuwakilishwa kwa mara ya kwanza bungeni

Vyama vya mrengo wa kulia havina nguvu za kumzuwia Pedro Sanchez asiunde serikali ya muungano, licha ya chama cha siasa kali za mrengo wa kulia Vox kuwakilishwa kwa mara ya kwanza  na watu 24 bungeni. Miaka mitatu iliyopita chama hicho cha siasa kali za mrengo wa kulia Vox kinachoongozwa na Santiago Abascal kilijipatia asili mia 0.2 tu ya kura, katika uchaguzi wa jana kimejikingia zaidi ya asili mia 10. Hii ni mara ya kwanza tangu utawala wa kifashisti wa jenerali  Franco ulipomalizika mwaka 1975 kwa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia kuwakilishwa bungeni nchini Uhispania.

Wahafidhina wa chama cha Umma PP wamepoteza nusu ya viti walivyokuwa wakividhibiti na kubakiwa na wabunge 66 dhidi ya 137 mnamo mwaka 2016. Waliberali wa Ciudadanos watawakilishwa na wabunge 57 badala ya 32 waliokuwa nao kufuatia uchaguzi wa mwaka 2016.

Kwa jumla kizungumkuti kiko vile vile kama kilivyokuwa kabla ya uchaguzi. Kuna mgawanyiko kati ya mrengo wa kushoto na mrengo wa kulia na hakuna hata upande mmoja wenye wingi wa kutosha wa kura.Vurugu huenda likaselelea.

 

Mwandishi: Riegert Bernd/Hamidou Oummilkheir

Mhariri: Mohammed Khelef

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com